Imam Hussein (a.s) hakukubali kusalimu amri mbele ya mtu mtu muovu kama huyo, kwa sababu Uislamu hauwezi kamwe kuongozwa na Kiongozi mwovu na fasiki kama Yazid bin Muawia (la).

5 Julai 2025 - 18:46

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Majlisi ya Tasu'a imefanyika Leo hii katika Chuo cha Al-Mustafa (s) - Nchini Malawi katika kuadhimisha Shahada ya Imam Hussein (as).  Khatibu wa Majlis hii alikuwa ni: Sheikh Talib Khamis Maduka. Na mada iliyozungumziwa ni: "Sababu ya Imam Hussein (as) Kukataa Kumuunga Mkono Yazid"

Majlisi ya Tasu’a – Chuo cha Al-Mustafa(s), Tawi la Malawi Sababu ya Imam Hussein (a.s) Kukataa Kumuunga Mkono Yazid + Picha

Katika Khutba yake ya siku ya Tasu’a (siku ya tisa ya Muharram), Sheikh Talib Khamis Maduka alieleza sababu kuu iliyomfanya Imam Hussein (a.s) kamwe asikubali kutoa kiapo cha utiifu kwa Yazid (la).

Imam Hussein (a.s) alijua vyema kuwa Yazid bin Muawia alikuwa mtu fisadi, aliyekuwa na sifa mbaya kupindukia kama vile:

1_Kuwa Mlevi wa pombe.

2_Mcheza kamari.

3_Alikijihusisha pia na mambo ya ushoga.

4_Alikichezea Wanawake hadharani.

5_Alikifanya madhambi kwa uwazi na bila haya.

Majlisi ya Tasu’a – Chuo cha Al-Mustafa(s), Tawi la Malawi Sababu ya Imam Hussein (a.s) Kukataa Kumuunga Mkono Yazid + Picha

Baada ya kuuawa kwa Imam Hussein (a.s), wafuasi wa Yazid waliandaa sherehe kubwa ambapo walikunywa pombe kwa wingi kama ishara ya kusherehekea mauaji hayo ya kinyama dhidi ya Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Majlisi ya Tasu’a – Chuo cha Al-Mustafa(s), Tawi la Malawi Sababu ya Imam Hussein (a.s) Kukataa Kumuunga Mkono Yazid + Picha

Imam Hussein (a.s) hakukubali kusalimu amri mbele ya mtu mtu muovu kama huyo, kwa sababu Uislamu hauwezi kamwe kuongozwa na Kiongozi mwovu na fasiki kama Yazid bin Muawia (la).

Majlisi ya Tasu’a – Chuo cha Al-Mustafa(s), Tawi la Malawi Sababu ya Imam Hussein (a.s) Kukataa Kumuunga Mkono Yazid + Picha

Khutba hii ilikuwa sehemu ya maadhimisho ya Tasu’a yaliyoandaliwa na Tawi la Jamiat Al-Mustafa (s.a.w.w) nchini Malawi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha